Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Muhammad Shehbaz Sharif, Waziri Mkuu wa Pakistan, katika ujumbe wake alimpongeza Ayatollah Sayyid Mujtaba Khamenei kwa kuchaguliwa kuwa Kiongozi wa tatu wa Mapinduzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Matini ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:
Ningependa kwa mara nyingine tena kuwasilisha rambirambi zangu za dhati pamoja na dua za moyo wote za wananchi wa Pakistan kufuatia kuuawa kishahidi kwa baba yenu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei (ra), Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Bila shaka huu ni wakati wa huzuni na mgumu kwa watu, ndugu wa Iran na pia kwa Umma wa Kiislamu. Katika kipindi hiki nyeti, kupandishwa kwenu katika nafasi ya uongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kumeleta fursa ya kipekee na isiyo na mfano.
Waziri Mkuu wa Pakistan alisisitiza: Nikiwasilisha pongezi zangu za dhati kwako kwa kukubali jukumu hili kubwa, ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu akujaalie muliongoze taifa lenu katika siku zijazo kuielekea amani, utulivu, heshima na ustawi.
Aliongeza kuwa: Mahusiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Pakistan na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yamejengwa juu ya msingi wa imani, lugha, utamaduni na historia ya pamoja. Tutaendelea na ushirikiano wa karibu ili kuimarisha zaidi mahusiano katika nyanja zote zenye maslahi ya pamoja, kwa manufaa ya mataifa yetu mawili.
Shehbaz Sharif alihitimisha kwa kusema: Ninakuombea afya njema, furaha na mafanikio. Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu akulinde wewe na wananchi, ndugu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na awajalie baraka zake.
Maoni yako